Saturday, July 18, 2020

Rais Magufuli amemteua Dk Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu

Rais John Magufuli amemteua Dk. Mwinyi Talib Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Haji alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi.

Uteuzi wa Dk. Haji unaanza leo Julai 18, 2020 na anatakiwa kuwepo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Julai 20, 2020 majira ya saa 4:00 asubuhi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/18/rais-magufuli-amemteua-dk-haji-kuwa-naibu-katibu-mkuu/

No comments:

Post a Comment