Saturday, July 18, 2020

Polepole: Tukipata viongozi wasiotosheka ni shida atakuacha mtoni tutawaangalia kama alituvusha

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema sifa mojawapo ya kiongozi wa CCM ni kutosheka.

“Ukiambiwa umepata sema asante na ukiambiwa umekosa  pia unasema asante,” alisema Polepole.

Polepole alisema kuna watu wameteuliwa na Rais John Magufuli tangu mwaka 2015 na kwa sasa wamefikia kwenye mto wanaondoka.

“Chama hiki kikipata viongozi wasiotosheka ni shida, mtu asiyetosheka ukimpa kazi hii atakuacha mtoni, ukimpa nyingine atakuacha mtoni. Tukifika kwenye chama kule tutaangalia kama alituvusha kwenye mto ama hakutuvusha,”



source http://www.bongoleo.com/2020/07/18/polepole-tukipata-viongozi-wasiotosheka-ni-shida-atakuacha-mtoni-tutawaangalia-kama-alituvusha/

No comments:

Post a Comment