Saturday, July 18, 2020

Rais Magufuli amefanya mabadiliko kwa uteuzi alioufanya Julai 17, 2020

 

Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya uteuzi alioufanya Julai 17, 2020 ambapo amemteua mhandisi Marwa Mwita Rubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kabla ya uteuzi huo, mhandisi Rubirya alikuwa meneja wa wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) katika mkoa wa Mwanza.

Mhandisi Rubirya ameteuliwa badala ya JumanneFhika ambaye atabaki ofisi ya Rais kuendelea na majukumu yake.

Uteuzi wa Mhandisi Rubirya umeanza leo Julai 19, 2020 na anatakiwa kuwepi Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma kesho majira ya saa 4:00 asubuhi.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/19/rais-magufuli-amefanya-mabadiliko-kwa-uteuzi-alioufanya-julai-17-2020/

No comments:

Post a Comment