Saturday, July 18, 2020

Dondoo za leo: Binti (19) ashikiliwa mauaji ya mwanafunzi wa chuo, CCM yatishia kufuta wagombea wote na Kanali atinga na Mkokoteni kuchukua fomu

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai upo salama.

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Binti wa miaka 19 ashikiliwa mauaji ya mwanafunzi wa chuo, CCM kufuta wagombea wote na Kanali atinga na Mkokoteni kuchukua fomu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SUZY KENNETH KASITEJETA [19] Mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya LINUS JAMES MAGESA [21] Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya [MUST] Kitengo cha Biomedical mwaka wa kwanza na Mkazi wa Ikuti kwa kumchoma kitu chenye ncha kali kifuani.

Ni kwamba mnamo tarehe 17.07.2020 majira ya saa 22:00 Usiku huko eneo la Ikuti lililopo Kata na Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya SUZY KENNETH KASITEJETA [19] na LINUS JAMES MAGESA [21] ambao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi waligombana na kupelekea LINUS JAMES MAGESA kujeruhiwa sehemu za kifuani kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali na SUZY KENNETH KASITEJETA hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu.

Leo tarehe 18.07.2020 majira ya saa 00:05 Usiku LINUS JAMES MAGESA [21] alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa wapenzi hao walikuwa wakigombana mara kwa mara. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Soma zaidi>>>

CCM YATISHIA KUFUTA WAGOMBEA WOTE

Mbunge aivaa CCM | Zanzibar, Kwanza, ChamaCHAMA cha Mapinduzi ( CCM) mkoani Shinyanga kimetishia kuwafuta wanachama wake wote wanaotaka kuwania jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi yake kutokana na baadhi yao kuwatembelea majumbani wapiga kura ndani ya chama na kuonesha dalili za kutoa rushwa.

Idadi kubwa ya watia nia ni vijana na robo tatu wanaelimu ya Shahada na wapiga kura za maoni ndani ya chama ni 449.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa alipokuwa katika kikao cha dharura na waombaji 60 wa jimbo la Shinyanga mjini na kuwaeleza kuwa mienendo ya wengi wao imekuwa siyo mizuri .

Soma zaidi>>>

KANALI ATINGA NA MKOKOTENI KUCHUKUA FOMU

Kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kichonge Mahende Masero, ambaye ametia nia ya kugombea jimbo la Tarime Mjini alizua gumzo akiwa anachukua fomu na kuirejesha akiwa kwenye usafiri wa mkokoteni.

Masero ambaye ni kada wa CCM Ijumaa Julai 17, 2020 wakati akirejesha fomu alitumia usafiri wa toroli huku bodaboda zikimsindikiza.

Soma zaidi>>>

Kumalizia dondoo zetu, tuangazie atizo la kupata choo kigumu.

Constipation (Mobile Bay Parents) - Children's Medical GroupJe wajua kwamba kupata choo kigumu kwaweza kukusababishia kupoteza Fahamu? Norman Jonas, Daktari na mtaalamu wa masuala ya Afya ya JAmii anafafanua hili.

Dk. Norman anasema Inawezekana kupoteza fahamu kutokana kujisaidia Choo hasa Choo kigumu, hali inayotambulika kama Defecation Syncope na ni adimu sana.

Anafafanua kuwa, hali ya kupoteza fahamu hutokana na choo kinavyotoka kusisimua mwitiko wa neva unaoitwa vasovagal na kusababisha mapigo ya moyo na presha kushuka ghafla na mtu kupoteza fahamu.

Ni hayo tu kwa leo mdau wetu, endelea ku2habarika na Opera News, asante na siku njema.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/19/dondoo-za-leo-binti-19-ashikiliwa-mauaji-ya-mwanafunzi-wa-chuo-ccm-yatishia-kufuta-wagombea-wote-na-kanali-atinga-na-mkokoteni-kuchukua-fomu/

No comments:

Post a Comment