Sunday, July 19, 2020

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa matukio ya moto yaliyotokea shule za Dar

Jeshi la Polisi limesema linaendelea na  uchunguzi ili kubaini vyanzo vya moto vilivyotokea katika shule zilizoungua jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Jeshi la Polisi , David Misime

“Kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia matukio ya moto ambayo yamepelekea kuunguza shule ya sekondari ya Ilala Islamic mnamo Julai 04, 2020 na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu, Kinondoni Muslim Julai 17, 2020 na Mivumoni moto uliteketeza darasa na jana Julai 18, 2020,”

Taarifa  hiyo ilieleza kuwa matukio haya ni wazi yameleta taharuki na maswali mengi kwa jamii kuhusiana na namna matukio yanavyojitokeza kwa mfululizo.

“Vyombo vya dola vinaendelea kufanya uchunguza ili kuweza kubaini vyanzo vya moto huo vilivyosababisha vifo, hofu kwa wafanyakazi, wanafunzi, wazazi, walenzi pamoja na kusababisha  hasara kubwa,” alisema.

Wakati uchunguzi ukiendelea jeshi linatoa wito kwa kila mmiliki na viongozi wa shule kuendelea kuchukua tahadhari na kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa kuwatumia wataalamu wa masuala ya moto katika sheria na kanuni zinavyoelekeza kwa majengo ya taasisi za elimu na taasisi za utafiti.

“Pia swala la ulinzi kila mmoja alitazame upya ili kuimarisha zaidi pale ambapo umelegalega,” alisema



source http://www.bongoleo.com/2020/07/19/jeshi-la-polisi-linaendelea-na-uchunguzi-wa-matukio-ya-moto-yaliyotokea-shule-za-dar/

No comments:

Post a Comment