Wednesday, July 15, 2020

Mwanasheria wa NEMC amechukua fomu ya kugombea ubunge ataka kumng’oa Ester Matiko

 

Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche, amechukua fomu ya kuomba kuwania ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM).

Heche amechukua fomu hiyo leo huku akisema lengo lake ni kutaka kuisaidia serikali ya awamu ya tano pamoja na kukomboa majimbo ambayo yamechukuliwa na upinzani likiwemo la Tarime Mjini.

Jimbo hilo lilikuwa linashikiliwa na aliyekuwa mbunge kutoka upinzani Ester Matiko.

Matiko amechukua fomu ya kutetea jimbo hilo aliloliongoza kwa miaka mitano.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/mwanasheria-wa-nemc-amechukua-fomu-ya-kugombea-ubunge-ataka-kumngoa-ester-matiko/

No comments:

Post a Comment