Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania nchini Shiekh Issa Ponda amekamatwa na jeshi la polisi kwa mahojiano juu ya walaka wa uchochezi aliolitoa hivi katibuni.
Akizungumza baada ya kuthibitisha kumkamata katibu huyo, Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema wamemkamata baada ya kuona andiko hilo.
“Tunaye sisi Polisi, tumemkamata kwa Mahojiano ya Uchochezi walioutoa kwenye kitu walichokiita Waraka. Tunamhoji kutokana na ule Waraka, Yeye kakubali kwamba ni wake na Taasisi yake lakini Viongozi wote wa Taasisi wameukana”amesema.
Ikumbukwe mnamo mwaka 2013 katibu huyo wa jumuhiya ya waislam alishikiliwa na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani kutokana na kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili ya uchochezi.
"Tunaye sisi Polisi, tumemkamata kwa Mahojiano ya Uchochezi walioutoa kwenye kitu walichokiita Waraka. Tunamhoji kutokana na ule Waraka, Yeye kakubali kwamba ni wake na Taasisi yake lakini Viongozi wote wa Taasisi wameukana” – Kamanda Mambosasa kuhusu Polisi kumkamata Sheik Ponda
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) July 11, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/12/polisi-ythibitisha-kumshikilia-sheikh-ponda/
No comments:
Post a Comment