Wednesday, July 15, 2020

Ndumbaro Atinga Kuchukua Fomu na Baiskeli

Image

Zoezi la uchukuaji fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kwenye nyadhifa mbalimbali ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) unaendelea kote nchini mpaka kufika Julai 17,2020.

Leo Julai 15,2020 Naibu Waziri wa mambo ya nje ya Dkt.Damas Ndumbaro ametia fola kwa kufika kwenye ofisi za CCM mkoani Ruvuma kwa kutumia baiskeri kwa ajili ya kuchukua fomu.

Ndumbaro ambaye ni mbunge wa jimbo ka Songea mjini kupitia CCM anayemaliza muda wake anakuwa mmoja kati ya wagombea wengi wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mbunge.

Miezi kadhaa iliyopita rais Magufuli alieleza namna naibu waziri huyo alivyopenya kwenye mchakato wa kupita kwenye kinyanganyiro cha kuwa mbunge muula wa kwanza mwaka 2015.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/ndumbaro-atinga-kuchukua-fomu-na-baiskeli/

No comments:

Post a Comment