Wednesday, July 15, 2020

Diamond Atangaza kumkwachua Kipenzi Mpya Baada ya Kumtema Tanasha Donna

Tanzania Star Singer Diamond Platnumz Dating Kenyan Radio ...

Mondi ameeleza kuwa amechoka na kuhusika katika mapenzi nje ya ndoa. Picha: Hisani

Diamond Platnamz ametangaza kuhusu mpango wa kufunga pingu za maisha miezi michache ijayo.

Mondi ameeleza kuwa amechoka na kuhusika katika mapenzi nje ya ndoa.

Ameeleza kuwa tayari amepata kipenzi na kuwa Tanasha Donna hayuko tena kichwani mwake

Msanii tajika wa Bongo Diamond Platnumz hatimaye ametangaza wazi kuwa amepata kipenzi mwengine miezi mitano baada ya kuonyeshana kisogo na Tanasha Donna.

Diamond ameeleza kuwa yuko katika uhusiano na mpenzi mwengine na kuwa hivi karibuni atafunga pingu za maisha naye anaposherekea umri wa miaka 31.

Baba huyo wa watoto watano amesisitiza kuwa amechoka na maisha ya kuchovya asali ya nje, hivyo yuko tayari kumuoa mwanadada huyo ili kuwa na mzinga rasmi.

‘’ Nina mwanamke mrembo ninayetaka kumuoa. Hivi sasa sitafuti mikiki tena, nataka kuoa,’’ Diamond alisema.

Aidha alisema ifikapo Disemaba atafikisha umri wa miaka 31 na hatataka kutajwa kama mume ambaye anawapenda makahaba.

Msanii Diamond na Tanasha Donna walitengana Februari 14, 2020 baada ya kuwa na changamoto katika uhusiano wao kwa zaidi ya miezi sita. Tanasha akijitoeza kueleza kuwa aliwafanya kila juhudi kutia kiraka uhusiano wao lakini maziwa yalikuwa yamemwagika.

View this post on Instagram

SIMBA LA KIMASAI…..🦁

A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on

Kulingana na Msanii Diamond, waliamua kuuvunja uhusiano wao maana hawakuweza kukubaliana kuhusu baadhi ya masuala ya kimsingi ambayo ni nguzo ya ndoa.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/diamond-atangaza-kumkwachua-kipenzi-mpya-baada-ya-kumtema-tanasha-donna/

No comments:

Post a Comment