Friday, July 17, 2020

Mwanamke Kortini kwa Kumshambulia Polisi Kituoni

Makadara law courts 5

Afisa huyo alisalia kinywa wazi asijue la kufanya kabla maafisa wenza kufika upesi kwa msaada wake. Picha: Hisani.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa makamo amejipata pabaya baada ya kufika katika kituo cha polisi kuripoti kesi yake.

Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika jarida la Nairobian, Mwanamke huyo aliyetambulika kama Faith Wangui Kinyanjui alifika katika mahakama ya Makadara Julai, 15 kuhusu kesi aliyoripoti awali, kisa ambako alidai kuwa jirani yake alikuwa amempiga.

Katika harakati ya kuandikisha taarifa yake, Emily Ndiwa ambaye ni afisa wa kituo hicho alimuomba kuleta taarifa ya shahidi katika kesi yake swala ambalo alidinda kabisa kufanya akidai kwa maafisa hao walikuwa na nia ya kummzungusha bure asipate haki.

Faith alidai kuwa afisa huyo hakutaka kufanikisha kesi yake na hivyo akashikwa na hasira na kuanza kumnyoshea afisa huyo kidole kwa hasira tayari kumvamia huku akipiga kelele.

Alternative justice systems can temper State monopoly on law ...

Faith aliyakana madai ya kumtishia afisa huyo wa polisi na kuachiliwa kwa dhamana. Picha; Hisani

Afisa huyo alisalia kinywa wazi asijue la kufanya kabla maafisa wenza kufika upesi kwa msaada wake.

Faith alikamatwa na maafisa wengine waliokuwa karibu na kurushwa korokoroni kabla kufikishwa mbele ya hakimu kujibu mashtaka ya kuhatarisha maisha polisi.

Akiwa mbele ya hakimu, Faith aliyakana madai ya kumtishia afisa huyo wa polisi na kuachiliwa kwa dhamana ya Tsh 60,000 huku kesi hiyo ikitarajiwa kuanza kusikizwa Novemba, 28.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/mwanamke-kortini-kwa-kumshambulia-polisi-kituoni/

No comments:

Post a Comment