Saturday, July 11, 2020

Mrema asema watafanya kampeni kuhakikisha kura zinakwenda kwa Magufuli

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Mrema, amesema wataendelea kufanya kampeni nchi nzima kuhakikisha kura zinakwenda kwa Rais John Magufuli.

“Tutafanya kampeni nchi nzima kuhakikisha kura zote zinakwenda kwa mgombea urais wa CCM, Rais John Magufuli”

Aidha, amesema Mei 04, 2020 chama chake TLP  kilikutakana na kujadiliana nani atuongoze kwenye uchaguzi mkuu.

“Halmashauri Kuu ikasema hatuna mbadala wa Rais Magufuli, tukasema Magufuli anatosha, tukakutana tena Mei 08, 2020 kura zote zikamuangukia Rais Magufuli”



source http://www.bongoleo.com/2020/07/11/mrema-asema-watafanya-kampeni-kuhakikisha-kura-zinakwenda-kwa-magufuli/

No comments:

Post a Comment