Saturday, July 11, 2020

Fatma Karume: Kura ya Rais Zanzibar inaoigwa na wazazibari na sio Dodoma

Wakili wa Kujitegemea, Fatma Karume, amesema anavyoelewa suala la kupitishwa mgombea urais Zanzibar huko Dodoma kazi kubwa ipo kwenye kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu.

“Nilivyoelewa Mimi issue si kupitishwa Dodoma, Mgombea CCM wa Urais wa Zanzibar. CCM wana Haki yao kupitishwa mgombea wako hata kwenye vikao Jehanam,” aliandika fatma katika ukurasa wake wa twitter.

“ISSUE ni : Kura za Rais wa Zanzibar zinapigwa na wazanzibari na matakwa yao lazima yaheshimiwe,” aliandika Fatma.

Fatma alisema bila hilo Rais wao atakuwa anachaguliwa na Dodoma na si Zanzibar.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/11/fatma-karume-kura-ya-rais-zanzibar-inaoigwa-na-wazazibari-na-sio-dodoma/

No comments:

Post a Comment