Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewaomba Watanzania watakaopiga kura wamchague Rais John Magufuli bila kuharibu kura.
“Niwaombe wana CCM mtakapopiga kura pigeni zote kwa Magufuli bila ya kuharibu ili tumpe faraja. Kuelekea uchaguzi mkuu Niwaombe tufanye kazi kwa ushirikiano, bidii na tukatafute kura za Magufuli,” amesema Kinana
Aliongezea kuwa “Hakuna uchaguzi mwepesi. Sina mashaka hata kidogo, Magufuli atapata kura nyingi kuliko zile za mwaka 2015,”
Kinana amesema mwaka huu wa uchaguzi watapata wabunge wengi pamoja na madiwani.
“Tuzike tofauti zetu na tukiweke chama mbele kuliko maslahi yetu”. Amesema Kinana.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/11/kinana-sina-mashaka-na-magufuli-atapata-kura-nyingi-kuliko-zile-za-mwaka-2015/
No comments:
Post a Comment