Monday, July 20, 2020

Mrema Aitaka Tume Ya Uchaguzi Kumchukulia Hatua Dkt Mwinyi

CHADEMA Tanzania on Twitter: ""Leo tunapozungumza viongozi ...Mkurugenzi wa mawasiliano, itikadi, uenezi na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema ameitaka tume ya uchaguzi Zanzibar kuchukulia hatua mgombea wa urais kwa tiketi chama cha mapinduzi Zanzibar , Dkt Hussein Mwinyi kutokana na kuanza kampeni kabla ya muda.

Mrema amesema hayo leo kwenye ujumbe aliotuma kwenye ukrasa wake wa Twiiter na kudai kuwa vitendo anavyofanya kwa sasa Dkt mwinyi ni kampeni ambazo hajifunguliwa bado kwa vyama vingine.

“Tume ya uchaguzi Zanzibar imetangaza lini kuanza kwa Kampeni?  sheria zinakiukwa na hakuna wa kukemea. Msajili wa vyama anahangaika na kutishia vyama vya upinzani tuu huku akiwaacha CCM wakiendelea kuvunja Sheria na Katiba ya nchi” amesema Mrema.

Ikumbukwe kuwa Dkt Mwinyi alifanya ziara kwenye visiwa vya Pemba baada ya kuchaguliwa na chama hicho kuwakilisha kwenye uchaguzi ujao wa kitaifa.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/mrema-aitaka-tume-ya-uchaguzi-kumchukulia-hatua-dkt-mwinyi/

No comments:

Post a Comment