Thursday, July 16, 2020

Mfanyakazi wa benki ya Barclays afikishwa mahakamani kwa wizi wa Sh milioni 64

Mfanyakazi wa benki ya Barclays ,Gabrie Tesha (35) mkazi wa Tabata kinyerezi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi akikabiliwa na wizi wa Sh milioni 64.

Kesi hiyo imefikishwa leo katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, na kusomewa mashtaka yake mawili na Mwendesha Mashtaka Wonkyo Simon.

Simon alidai kuwa Oktoba 01, 2017 na Mei 31, 2018 maeneo ya benki ya Barclays akiwa mfanyakazi wa benki aliiba Sh milioni 64 kupitia miamala mbalimbali.

Katika shtaka la pili la utakatishaji fedha ilidaiwa tarehe hiyo hiyo katika eneo la benki hiyo alijihususha na miamala mbalimbali ya Sh milioni 64 ya kuingiza na kutoa katika akaunti yake ya taslimu na Dola wakati akijua fedha hizo ni zao la wizi.

Upelelezi wa kesi haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 29, 2020.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/mfanyakazi-wa-benki-ya-barclays-afikishwa-mahakamani-kwa-wizi-wa-sh-milioni-64/

No comments:

Post a Comment