Thursday, July 16, 2020

Mpoki Ajitosa Ubunge, Kuchuana na Makonda Kigamboni

Mchekeshaji wa muda mrefu na mtangazaji wa redio Sylvester Mjuni amekuwa mmoja kati ya wasanii waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa jimbo la Kigamboni jijini Dar es salaam.

Sylvester mjuni (Mpoki) amejitokea kwenye ofisi ya ccm wilaya ya Kigamboni kuchukua fomu hiyo ikiwani siku moja kabla ya zoezi hilo kufungwa rasmi na mchakato. wa ndani wa chama kuanza kuchuja wagombe hao.

Kwa mujibu wa taaairfa iliyotolewa leo na Rais John Magufuli leo julai 16,2020 mkoa wa dar es salaam unajumala ya wagombea 825 huku wanaccm walijitokea kuchukua fomu nchi nzima wakifika zaida ya 8000.

Baadhi ya wasanii wengie waliojitokeza kuchua fomu za kugombea kwenye chama cha mapinduzi ni pamoja na Steve Mangere (Iringa mjini), Jacob Mkweche (Liuli vijini) na Rashid Mwishehe.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/mpoki-ajitosa-ubunge-kuchuana-na-makonda-kigamboni/

No comments:

Post a Comment