Thursday, July 16, 2020

Membe: CCM Na Ujanja Wote Haijawahi Kumshinda Maalim Seif Zanzibar

Mwanachama mpya wa chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe ameweka wazi kuwa chama cha mapinduzi hakijawahi kushinda uchaguzi wowote ule wa Zanzibar tangu maalim seif alipoabza kugombea kupitia chama cha CUF.

Akizungumza leo wakati anatambulishwa rasmi kwenye chama hicho amesema licha ya CCM kuwa wajanja na kujua mambo mengi haijawahi kushida na haitokuja kumshinda Maalim upande wa Zazibar.

“CCM Pamoja na ujanja wetu wote Pemba hatujawahi kuichukua na hatutokuja kuichukua hata siku moja na Maalim ni mjanja hatari kwenye siasa za sasa anauwezo wa kuchukua wilaya na mikoa yote ya kisiwa cha pemba na huku unguja anatikisa yeye sasa cha kujivunia sasa hivi vyote anavichukua” amesema Membe.

Ikimbukwe siku kadhaa zilizopita katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Bahiru Ally alinukuliwa akisema hawawezi kuogopa uwepo wa maalim kwakua ni ntu aliyezoea kushindwa.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/membe-ccm-na-ujanja-wote-haijawahi-kumshinda-maalim-seif-zanzibar/

No comments:

Post a Comment