Thursday, July 16, 2020

Covid19: Rais wa Malawi Amfuata Magufuli, Aagiza siku 3 za Kufunga na Kuomba

Coronavirus: Born again Malawi president Lazarus Charekwa declares 3 days of fasting, prayer

Taifa hilo pia litachukua fursa hiyo kuwaombea wahudumu wa afya. Picha; Hisani.

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera aliwaomba wananchi wake wote kufunga siku tatu na kuwaombea wagonjwa na wahudumu wa afya waliambukizwa corona

Chakwera ambaye ni mkristo sugu alisema kuwa nchi hiyo itatumia muda huo kumshuru Mungu kwa aliyoitendea Malawi kwa miezi 12

Malawi hadi Alhamisi, Jalai 16 ilikuwa na takriban watu 2,614 walioambukizwa virusi vya corona, vifo 43 na 1,005 waliopona

Rais mpya wa Malawi Lazarus Chakwera amewaomba wanachi wake kutoka kila dhehebu kuungana naye katika siku tatu ya mfungo na maombi kufuatia mlipuko wa janga la corona nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya nchini humo Jumatano, Julai 15, madhumuni ya maombi hayo yatakuwa dhidi ya janga la virusi vya corona pamoja na kumshukuru Mungu kwa mazuri aliyoitendea nchi ya Malawi kwa mwaka mzima.

Siku hizo tatu za maombi yameanza hii leo Alhamisi, Julai 16 na itanatarajia kufikia kilele Jumapili 19 kwa maombi makuu ya shukrani.

‘’ Rais ameyaomba madhehebu yote na wakaazi wa Malawi kuungana naye katika siku tatu ya kufunga na kuomba dhidi ya virusi vya corona.  Rais pia amewaomba wanachi na wakaazi wote wa Malawi kuungana naye Jumapili, Julai 19 ikiwa ni siku ya kushukuru Mungu,’’ taarifa ya wizara ya afya.

Coronavirus: Born again Malawi president Lazarus Charekwa declares 3 days of fasting, prayer

Taifa hilo pia litachukua fursa hiyo kuwaombea wahudumu wa afya ambao wako katika mstari wa mbele katika kupamabana na virusi hivyo.

Hadi Alhamisi Julai 16, Malawi ilikuwa imerekodi visa 2,614 vya maambukizi, vifo 43 na 1,005 waliopona.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/covid19-rais-wa-malawi-amfuata-magufuli-aagiza-siku-3-za-kufunga-na-kuomba/

No comments:

Post a Comment