Sunday, July 19, 2020

Mashabiki wa Man U Wamtaja Mchezaji Nyota Wanayetaka Auzwe Baada ya Kuipa Chelsea Ushindi

David de Gea: Man United fans slam keeper after woeful performance against Chelsea

David de Gea amelaumiwa kuhusu magoli mawili waliofungwa

Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wamemtaka mlinda lango huyo kupewa mapumziko ya lazima

Chelsea iliicharaza Man U mabao 3-1 na kufuzu kuchuana na Arsenal katika fainali

Mashabiki wa klabu ya Manchester United hawana Amani haswa baada ya kuonyeshwa adabu na mahasimu wa jadi Chelsea katika mchuano wa nusu fainali Jumapili, Julai 19 katika uwanja wa Wembely.

Baadhi ya mahabiki hao sasa wamemkashifu pakubwa mlinda lango wa klabu hiyo David de Gea wakimtaja kama chanzo cha kupigwa na Chelsea.

Pindi tu baada ya kipindi cha kwanza, de Gea alifeli kuyazua mabao mawili ya wazi kabla ya Harry Maguire kuipa Chelsea bao la tatu kwa kujifunga.

Olivier Giroud aliipa Chelsea bao la ufunguzi dakika chache kabla kuisha kipindi cha kwanza huku Mason akitikisa wavu kwa bao la pili katika awamu ya pili.

Mashabiki wa klabu hiyo maarufu sasa wameshikilia kuwa de Dea amezidi kuwa ovyo na hata kuushauri usimamizi wa klabu hiyo kumuuza upesi.

‘’ De Gea asicheze tena msimu huu, kisha auzwe mwishoni mwa msimu,’’ mmoja alisema.

De Dea anastahili kuenda sasa. Nampenda lakini katika mechi hii ametuangusha kabisa.  Ametufaa pakubwa awali lakini katika msimu huu amekuwa mauzo tu,’’ mwengine alisema.

Baada ya Chelsea kupata fahari ya mabao 3-1 dhidi ya Man United, sasa wana kibarua kigumu katika kuthibitisha umahiri wao kwa mahasimu Arsenal katika fainali za FA.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/mashabiki-wa-man-u-wamtaja-mchezaji-nyota-wanayetaka-auzwe-baada-ya-kuipa-chelsea-ushindi/

No comments:

Post a Comment