Sunday, July 19, 2020

Dondoo za leo; Mbowe, Msingwa waingia mitini, Hakuna kuisoma namba nikishinda urais, Nimechoka lakini nitagombea

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba asubuhi na Mbowe, Msingwa waingia mitini, akishinda urais hakuna kuisoma namba adai na mwisho ni juu ya Lema kusema amechoka lakini atagombea.

MBOWE, MSINGWA WAINGIA MITINI

WANACHAMA wanne kati ya 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ‘wameingia’ mitini katika kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Wanachama hao walikuwa miongoni mwa 11 waliotia nia kuwania urais ndani ya chama hicho lakini hawakujitokeza kuchukua fomu pindi shughuli ya uchukuaji na urejeshaji ilipoanza tarehe 4 hadi 19 Julai 2020.

Soma zaidi>>>

NIKISHINDA URAIS HAKUNA KUISOMA NAMBA

LAZARO Nyalandu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati na mtia nia wa Urais kupitia chama hicho amesema, akiwa Rais wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaisoma namba.

Nyalandu ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 19 Julai 2020 wakati akirejesha fomu ya kukiomba chama hicho kimpitishe kuwa mgombea urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Soma zaidi>>>

NIMECHOKA LAKINI NAGOMBEA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (pichani) amesema mwili wake umechoka lakini nafsi yake inamsukuma aendelee kugombea ubunge jimboni humo.

Lema aliema kushinda kwake kwenye kura za maoni kunampa nguvu kupambana katika jimbo hilo ili aweze kupata kura nyingi awe Mbunge kwa mara ya tatu.

Soma zaidi>>>

Tukimalizia dondoo hebu tuangazie jambo hili la mdau anayeomba ushauri jinsi ya kuishi na Boyfriend wake mchafu;

Kuna mdau anaomba msaada wa namna ya kuishi na Mwanaume yaani ‘Boyfriend’ wake asiye na tabia ya usafi kuanzia mwilini hadi mahali anapokaa (ndani kwake)

Mdau anasema “Mimi sio mtu msafi sana ila Mwanaume huyu amenishinda. Ni mtu mzuri na nimekuwa naye kwa miezi 8 sasa, mwanzo sikuwa nimemuelewa ila huyu Mwanaume ni mchafu sana.”

Anaendelea “Akioga usiku kabla ya kulala asubuhi haogi. Yaani analala na Mwanamke usiku, asubuhi anaenda kazini hivyo hivyo. Hata nikisema hasikii wala haelewi, ndio kwanza anasema nampanda kichwani.”

Aidha, amesema “Chumba chake ndo kichafu usiseme. Kuna wakati nilisafiri kama mwezi hivi kurudi chumba hakitamaniki. Nikamsafishia na kila weekend nikawa naenda kusafisha. Nilipata ugeni na sikwenda kwake kama wiki mbili, nilivyoenda nilikuta sahani alizolia chakula siku kama 3 zilizopita zipo humo, machupa ya maji, maganda ya ndizi”

Mdau anaomba maoni yenu amfanye nini boyfriend wake aache hiyo tabia na je, anaweza kuishi naye vipi?



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/dondoo-za-leo-mbowe-msingwa-waingia-mitini-hakuna-kuisoma-namba-nikishinda-urais-nimechoka-lakini-nitagombea/

No comments:

Post a Comment