Monday, July 20, 2020

Makonda Apingwa Chini Kura Za Maoni Kigamboni

ImageAliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameshika nafasi ya pili kwenye mchakato wa ndani wa chama wa kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) kwenye jimbo la Kigamboni.

Kwenye uchaguzi huo ambao ulipingwa kura na jumla ya wajumbe kutoka kwenye wilaya aliyeongoza ni mbunge aliyemaliza muda wake Dkt.Faustine Ndungulile aliyepata jumla ya kura 190 huku mkuu huyu wa mkoa wa Dar es salaam aliyepita akipata kura 122.

Mchakato wa awali wa kuchagua wagombea wa chama kwenye uchaguzi mkuu ujao unaendelea kwenye maeneo husika ikiwa ni hatua awali kabla ya ngazi ya mkoa na taifa kupisha majina hayo na kuutangaza mshindi atakayepeperusha bendera ya chama kwenye uchaguzi.

Ikumbukwe mapema mnamo julai 15, 2020 mkuu huyo wa mkoa wa zamani alijitokeza kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya wagombea 800 walijitokeza jijini Dar es salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/makonda-apingwa-chini-kura-za-maoni-kigamboni/

No comments:

Post a Comment