Monday, July 20, 2020

Makonda hali tete kura za moani na Dk. Ndugulile aibuka kidedea kwa kura 190

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameambulia kura 122 sawa na asilimia 30 katika uchaguzi wa kura za maoni za ubunge katika jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dk. Faustine Ndugulile ameambua kura 190 sawa na asilimia 45 baada ya kutangazwa katika uchaguzi huo kuwa ni mshindi na zaidi ya wagombea 20 walipata kura za sifuri.

Mchuano huo katika kura za maoni unadaiwa kuwepo na ushindani mkali ni kwamba matokeo yalitangazwa majira ya saa 1:14 jioni.

Katika jimbo hilo walijitokeza wagombea 78 kuomba ridhaa ya kugombea jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na walipiga kura walikuwa 399.

Jimbo hilo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu matokeo yake ikilinganishwa na maeneo mengine huku wakitaka kujua nani mshindi kati ya Makonda na Dk Ndugulile.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/makonda-hali-tete-apata-kura-122-na-dk-ndugulile-aibuka-kidedea-kwa-kura-190/

No comments:

Post a Comment