Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Alhamisi Julai 09, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.
Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.
Habari hizo ni Lema na Heche kuchukua fomu leo za kugombea Ubunge wasema wanarudi katika majimbo yao, Waziri Mkuu amefariki dunia baada ya kutoa kwenye kikao cha baraza la mawaziri je unajua ni nani? na Uchebe asimulia mazito kuhusu Shilole kulikoni? je kuna kilichojificha nyuma ya pazia?
Karibu Msomaji wetu;
LEMA NA HECHE LEO KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE
Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, wametangaza kuchukua fomu leo ya kugombea katika majimbo yao waliyokuwa wanayaongoza.
Lema amesema leo majira ya saa tano atakwenda kuchukua fomu ya kuendelea kuwa mbunge wa Arusha Mjini 2020 hadi 2025.
WAZIRI MKUU AAGA DUNIA BAADA YA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 alikuwa amechaguliwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa mwezi Oktoba, baada ya Alessane Ouattara kusema kuwa hatowania muhula wa tatu.
Bwana Gon Coulibaly alikuwa amerudi kutoka Ufaransa ambapo alikuwa amepokea matibabu ya moyo kwa miezi miwili.
Rais Ouattara amesema kuwa taifa linaomboleza.
Alisema kwamba bwana Gon Coulibaly alianza kuhisi vibaya wakati wa kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri na akapelekwa hospitali ambapo alifariki baadaye.
UCHEBE AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SHILOLE
Ashrafu Sadiki maarufu kwa jina la Uchebe amesema picha ambazo amitupilia Mwanamuziki Zuena Mohammed maarufu kama Shilole katika mitandao ya kijamii akilalamikia kupigwa ni za muda mrefu kabla ya ndoa yao.
“Sijui kwa nini kafanya hivyo wanawake wasanii mtihani sana hizo picha ni za muda mrefu sana…. Hata kumuoa sijamuoa enzi hizo kipindi hicho Shilole hajaacha mambo yake,”
“Sio kwa sababu sina hela simtimizie mambo mengine ndio anidharau mimi eti vile ana hela viongozi wanamjua sio sahihi,”alisema Uchebe.
Alisema suala la kudai amempiga siku mbili sio taarifa za kweli kwani hajalala nyumbani siku mbili na hajui alipolala je atawezaje kumpiga.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/dondoo-za-leo-lema-na-heche-kuchukua-fomu-za-ubunge-waziri-mkuu-aaga-dunia-baada-ya-mkutano-wa-baraza-la-mawaziri-na-uchebe-asimulia-mazito-ya-shilole/
No comments:
Post a Comment