Thursday, July 23, 2020

Madagascar Taabani, Yaomba Msaada Kukabiliana na Corona Licha ya Kuzindua Tiba

https://www.google.com/url?sa=i&url=https%3A%2F%2Fwww.dnaindia.com%2Fworld%2Freport-covid-19-pandemic-madagascar-president-introduces-herbal-cure-for-coronavirus-2823577&psig=AOvVaw2kRHc1uLGXekGs8mjxQU5P&ust=1595574985856000&source=images&cd=vfe&ved=0CAIQjRxqFwoTCLjLxZnq4uoCFQAAAAAdAAAAABAD

Rais wa Madacacar Andy Rajoelina alizindua dawa ya kienyeji ya kutibu virusi hivyo Aprili, 2020. Picha: Hisani

Madagascar iliweka masharti makali kupambana na virusi vya covid19 katika jiji kuu la Antananarivo

Katika hospitali moja ya serikali mjini humo, mkurugenzi ameeleza kuwa wana wagonjwa 46 walioambukizwa corona na nafasi zilizosalia ni nne tu

Rais wa Madacacar Andy Rajoelina alizindua dawa ya kienyeji ya kutibu virusi hivyo Aprili, 2020

Maafisa wa afya nchini Madagascar wamelalamika kuhusu ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona, mahospitali zikikosa nafasi za kuwalaza watu zaidi walioambukizwa.

Waziri wa afya nchini humo amelazimka kuomba msaada kutoka katika mashirika ya nchi za nje kabiliana na hali hiyo.

Kulingana naye, Madagascar haiwezi kukabiliana tena na idadi ya maambukzi inayopanda kila siku, huku vifaa vya kutumika katika kuwahudumia wagonjwa hao vikiadimika.

Waziri huyo ameomba msaada wa vipumizi, glovu, vifaa vya vipimo pamoja na msaada wowote utakowafaa katika kubaliana na janga la corona.

Katika hospitali mmoja mjini Antananarivo, mkurugenzi alieleza kuwa walikuwa na wagonjwa 46 wa maradhi hayo na walikuwa na nafasi ya wanne pekee zimesalia.

Hadi Alhamisi, Julai 23, Madagascar ilikuwa imerekodi idadi ya maambukizi 8,162 na zaidi ya 80% zikiripotiwa mwaka jana.

Idadi ya maambukizi haya yanaongezeka maradufu licha ya Rais wa Nchi hiyo Andy Rajoelina kuzindua tiba ya kienyeji kwa maambukizi hayo Aprili 20, 2020.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/madagascar-taabani-yaomba-msaada-kukabiliana-na-corona-licha-ya-kuzindua-tiba/

No comments:

Post a Comment