Thursday, July 16, 2020

Lema: Wagombea CCM wamefurika utasema ni usajili wa darasa la kwanza

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamefuriki utafikiri kuna uandikishwaji wa darasa la kwanza.

Lema amesema aliyekuwa mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa, amemjulisha watia nia wa CCM wamefika 96.

“Mh Peter Msigwa ananiambia kwake watia nia CCM wamefika 96 na huku nafikiri kwa sasa wamefika pengine 80 yaani utafikiri kuna uandikishwaji wa darasa la kwanza,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa Twitter.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/lema-wagombea-ccm-wamefurika-utasema-ni-usajili-wa-darasa-la-kwanza/

No comments:

Post a Comment