Monday, July 13, 2020

KIsa cha Wanandoa Waliojaliwa Mapacha 3 Baada ya Kuishi kwa Miaka  21 Bila Mtoto

Githurai couple welcomes triplets after 21 years of barrenness

Hatimaye walijaliwa mapacha watatu. Picha: HIsani.

John na Florence walifanya kila nia kupata mtoto, kwa wakati mmoja walilazimika kutumia hadi zaidi ya TSh 6 milioni

Wawili hao walidumu kwa ndoa kwa miaka 21 bila dalili yoyote ya kupata mtoto

Hatimaye walijaliwa mapacha watatu

Sawa na hadithi ya Biblia ya Hannah, Wanandoa Wakenya wanaoishi katika mtaa wa Githurai, Florence Makena na mumewe John Gitobu wamehisi kuwa wameguswa na malaika baada kuishi miaka 21 wakilia usiku na mchana wakiombea baraka ya mtoto.

Wawili hao ambao waliweza kubanana pamoja kwa kila nia licha ya magumu na mazito kuwasonga hatimaye waliona mkono wa Bwana.

Si mmoja, si wawili bali walijaliwa mapacha watatu mara moja, hao ndio wakawa asante ya kusubiri kwa Imani.

Githurai couple welcomes triplets after 21 years of barrenness

Hawakupoteza matumaini hata baada ya miaa 21. Picha: Hisani

‘’ Baada ya miaka 21,Mungu ameamua kunibariki na kunimulikia mwanga.  Nilikuwa mja mzito  na kujifungua mapacha watatu,’’ Florence aliiambia KBC.

Wawili hao walijaliwa mtoto wa kwanza lakini kwa bahati mbaya akafariki wakati wa kuzaliwa, mama huyu alifanyiwa upasuaji na mtoto huyo akatolewa.

Githurai couple welcomes triplets after 21 years of barrenness

Baada ya miaka mitatu hawakuona dalili ya mtoto, ndipo wakaona haja ya kutafuta njia mbadala.

‘’ Tulikaa kwa muda na kutumia pesa nyingi hadi tukakosa la kufanya. Tuna madeni ya zaidi ya TSh  milioni,’’ John alisema.

Florece alijifungua mapacha watatu wa kiume na kumpa mmoja jina muujiza kama shukrani kwa Mungu.

Wawili hao sasa wanamuomba yeyote ambaye ataweza kujitokea kuwasaidia katika kulipa deni ya TSh 6 milioni  walizochukua katika njia ya kutafuta mtoto.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/kisa-cha-wanandoa-waliojaliwa-mapacha-3-baada-ya-kuishi-kwa-miaka-21-bila-mtoto/

No comments:

Post a Comment