Monday, July 13, 2020

CCM Yawaonya Wanoatangaza Nia Mtandaoni

LIVE: HUMPHREY POLEPOLE ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI JUNE 2, 2020 ...Katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi Humprey Polepole amewataka wananccm wanatumia vipeperushi mtandaoni wakijitangaza nia za kugombea kuacha mara moja.

Alizumgumza leo Julai 13, 2020 na wanahabari mjini Dodoma Polepole amesema kitendo hicho ni kinyume na sheria za chama kwakua wapo wasio na uwezo wa kujinadi kwa vipeperushu vya mtandaoni hali inayoleta matabaka.

“Kuna ambao wameshaanza kutumia mabango na vipeperushi mtandaoni wakitangaza nia ya kugombea nawaambia ni kosa kwa mujibu wa katiba ya chama, kamati za siasa za eneo husika wawakataze na kuwakataza waache mara moja na watakao kataa kuacha tutatafuta namna ya kuwafanya” amesema Polepole.

Ikumbukwe kuwa chama cha Mapinduzi (CCM) inaanza rasmi mchakato wa kugawa fomu za udiwani, Ubunge na uwakilishi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/ccm-yawaonya-wanoatangaza-nia-mtandaoni/

No comments:

Post a Comment