Tuesday, July 14, 2020

Kisa cha Mwizi Aliyeiba Gari na Mtoto Ndani na Kulazimika Kurejesha Mtoto, Uhondo kamili

Meet a man who stole a car with a baby inside and brought the ...

Jamaa huyo aliliaba gari hilo huku wenya gari hilo wameingia katika duka la jumla kufanya ununuzi

Aligundua kuwa gari hilo lilikuwa na mtoto katika kiti cha nyuma baada ya mtoto huyu kuanza kulia

Alirudisha gari hilo upesi na kuwakabidhi wawili hao mtoto wao

Wanavyosema waswahili, kuishi kuishi kingi kuona mengi, kisa kimoja cha ajabu kimetendeka nje ya duka moja la jumla Marekani mwizi akilazimika kugeuka msamaria mwema.

Katika kisa hicho ambacho kiliwaacha wengi vinywa wazi,  mwizi mmoja alilazimika kurejesha gari aliloliiba, gari lenyewe likiwa na mtoto ndani.

Inadaiwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo waliliegesha gari wakiingia kwenye duka hilo kufanya ununuzi na kumuacha mtoto akilala humo.

Mwizi huyo ambaye alikuwa na nia ya kuliaba gari hilo mara moja baada ya kugundua kuwa wawili hao wamezama dukani, aliitumia ujuzi wake na kuingia kwenye gari hilo na moja kwa moja akaanza kuendesha upesi .

Baada ya kuenda kwa muda, dereva mwizi aligundua kuwa mtoto alikuwa amelazwa katika kiti cha nyuma baada ya mtoto huyu kuanza kulia kwa hasira.

Jamaa huyo alichanganyikiwa kuhusu la kufanya, kwa njia isiyo ya kawaida, jamaa huyo alilazimika kulirejesha gari hilo hadi alikolichukua baada ya kushindwa kuhimili kelele ya mtoto.

Alipowasili, aliegesha gari na kuchukua mtoto huyo hadi ndani ya duka hilo kuwatafuta wazazi wake. Aliwaambia kuwa walisahau kufunga mlango wa gari lao na kuwa mtoto wao alikuwa akilia na ndipo akaamua kumsaidia.

Wanandoa hao walimpongeza pakubwa kwa kumuokoa mwanao pasi kujua kuwa huyo alikuwa mwizi na kuwa mwano ndiye aliyeliokoa gari lao.

Maajabu hayaishi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/kisa-cha-mwizi-aliyeiba-gari-na-mtoto-ndani-na-kulazimika-kurejesha-mtoto-uhondo-kamili/

No comments:

Post a Comment