Tuesday, July 14, 2020

Fatma Karume Awashukia Polisi “Mbona Hamkukamata Wachungaji”


Aliyekuwa rais wa chama cha mawakili Tanganyika (TLS) Fatma Karume amehoji kitendo cha katibu ya jumuiya za Kiislam nchini Sheikh Issa Ponda kukamatwa kwa kutoa waraka wakati wapo waliotoa waraka wao na bado hajakamtwa.

Karume amehoji hayo kwenye ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa twitter na kudai kuwa mbona Wachungaji hawakukamatwa na walitoa waraka.

“Wachungaji walitoa WARAKA wao, Hakuna hata moja wao aliyekamatwa kwa WARAKA ule.  Haya tuendelee tu! Hamjambo?” Ameandika Karume.

Ikumbukwe kuwa mapema siku ya jumamosi Julai 11,2020 jeshi la polisi kanda maalim Dar Es salaam likitangaza kumkamata katinu wa jumuiya ya kiislam nchini kwa kusambaza waraka wenye ujumbe wa uchochezo.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/fatma-karume-awashukia-polisi-mbona-hamkukamata-wachungaji/

No comments:

Post a Comment