Sunday, July 19, 2020

Waziri Mkuu: Serikali imetoa Sh bilioni 20 kwa ajili ya kulipa madeni ya wakulima

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imetoa Sh bilioni 20 kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapulizaji dawa na waendesha maghala ya korosho wa Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti .

Fedha hizo ni kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa.

“JPM  ametoa hizi fedha kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa waliolipwa nusu, kiasi na wasiolipwa zitaanza kulipwa kesho,” amesema Waziri Mkuu.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/19/waziri-mkuu-serikali-imetoa-sh-bilioni-20-kwa-ajili-ya-kulipa-madeni-ya-wakulima/

No comments:

Post a Comment