Monday, July 13, 2020

Jamaa Ajitokeza kumtafutia Mamake Mchumba Mtandaoni

Man commences search for a companion for his mom

Ajibade Adedabo, alieleza kuwa alikuwa anajihitaji mume tajiri kumposa mamake. Picha: Hisani

Raia mmoja wa Nigeria, aliingia mtandaoni kumtafutia mamake ambaye ana umri wa miaka 60 mume wa kumuoa

Akijitambulisha kama Ajibade Adedabo, alieleza kuwa alikuwa anajihitaji mume tajiri kumposa mamake

Chapisho lake limeibua hisia mseto mtandaoni

Siku zote maisha ya mahusiano huwa na mambo ya kushangaza, mara nyingi swala nzima la uhusiano huwa ngumu kuelewa.

Je, umewahi kufikiri kuhusu mwanamke wa zaidi ya miaka 60 kujitokeza hadharani kutafuta mume? Hilo kando,  Katika kisa kilichowaacha wengi vinywa wazi, jamaa mmoja raia wa Nigeria ameitikisa mitandao baada ya kujitokeza hadharani kumtafutia mamake mwenye umri wa miaka 60 mume mtandaoni.

Katika chapisho lake kwenye mtandao wa twitter, bwana huyo aliyetambulika kama Ajibade Adedabo alipakia picha za mamake na kueleza kuwa alikuwa anamtafutia mume tajiri wa kumuoa, awe alitengana na mkewe ama hata kama mke alifariki.

‘’ Namtafutia mamangu mume, ana umri wa miak 60.  Iwapo una baba ambaye alipoteza mke ama walitengana, wasiliana nami, tunaweza kuwa madugu na dada,’’ aliandika katika ukurasa wake wa twitter.

Chapisho lake hili ambalo lilisambaa pakubwa liliwasha mitandao wengi wakimpongeza kwa kuwa na ujasiri huo, baadhi walimuuliza ni kwanini alihitaji mume tajiri na wala si mume yeyote tu.

Swala la kutafuta mpenzi mtandaoni si jambo geni tena  leo, kilichwashangaza wengi ni pale unapotafutiwa mume na mwanao. Je wewe waweza kukubali?



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/jamaa-ajitokeza-kumtafutia-mamake-mchumba-mtandaoni/

No comments:

Post a Comment