Monday, July 13, 2020

Dondoo za leo; Mgonjwa wa kwanza Corona kuishitaki serikali, Ahukumiwa kunyongwa, Lissu atoa neno

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni mgonjwa wa kwanza wa Corona kuishitaki serikali, Ahukumiwa kunyongwa na mwisho ni juu ya Lisu kutoa neno Membe upinzani.

MGONJWA WA KWANZA WA CORONA KUISHTAKI SERIKALI

Osman Shariff (62), mtu wa kwanza kuthibitika kuwa na maambukizi ya #CoronaVirus katika Kaunti hiyo amepanga kuiburuza Mahakamani Serikali ya Kaunti akiidai fidia ya Ksh. Milioni 25

Shariff amesema alipata matatizo makubwa ya kunyanyapaliwa na kupoteza wateja wengi katika biashara yake baada ya wafanyakazi wa idara ya afya kuweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii

Amewatuhumu wafanyakazi wa Hospitali ya Garbatula alipokuwa amelazwa katika eneo maalum (Karantini) kuwa walimpiga picha na baadaye kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii

Shariff amesema hivi sasa amepona kabisa #Corona ila bado anaugua zaidi maradhi ya kisaikolojia kwani watu wengi wameona picha yake kwenye mitandao ya kijamii na humnyanyapaa

AHUKUMIWA KUNYONGWA

Mkazi wa Katavi, Yustine Robert (35) amehukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga  baada ya kupatikana na hatia ya kumuuwa mke na watoto wawili.

Akisoma hukumu hiyo jana  Jaji Mfawidhi Wa Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga David Mrango, alisema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo katika eneo la majiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Aprili 5, 2013 kwa kuwatupa kwenye kisima cha maji mke wake na watoto wake wawili.

Soma zaidi>>>

LISSU ATOA NENO

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amezungumzia uamuzi wa Benard Membe kujiunga na upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika awamu iliyopita ya serikali, tayari ameshatangaza kujiunga na upinzani na mwishoni mwa wiki alikuwa na mazungumzo na uongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ambako inadaiwa atawania kiti cha urais kupitia chama hicho.

Soma zaidi>>>

Kumalizia dondoo hebu tuangalie jambo hili lililomkera mdau wetu juu ya watu kuwa na tabia ya kuwabusu watoto mdomoni.

Amesema, “Unakuta mtu kaja kutembelea mtoto wako au kamkuta umemshika anamchukua na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni. Huu ni uchafu sana mimi sipendi kabisa tabia hiyo”

Kimaadili tunaona haiko sawa sina hakika kama na wewe ungekipenda kitendo hicho.

Una maoni gani katika jambo hili?



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/dondoo-za-leo-mgonjwa-wa-kwanza-corona-kuishitaki-serikali-ahukumiwa-kunyongwa-lissu-atoa-neno/

No comments:

Post a Comment