Tuesday, July 14, 2020

Jamaa Ageuza Uwanja wa Shule kuwa Shamba la Mboga Kufuatia Mlipuko wa Covid19

Kirinyaga: School owner transforms playground into vegetable farm as COVID-19 effects persist

Alilazimika kugeuza uwanja wa shule hiyo kuwa shamba la mboga ili kupata mapato. Picha; Hisani.

Shule hiyo inayomilikiwa na James Kung’a ilifungwa tangu kisa cha kwanza cha covid19 kiliporipotiwa

Kungu ameeleza kuwa alitegemea karo za wanafunzi katika kufankisha shuhuli zake na kuendeleza shule hiyo.

Alilazimika kugeuza uwanja wa shule hiyo kuwa shamba la mboga ili kupata mapato

Mlipuko wa virusi vya corona viliathiri sekta kadhaa, shule zote zikifungwa, wamiliki wa shule za kibinafsi wakisalia mkono mtupu bila pato.

Hatua hii ilimfanya James Kung’a,mmiliki wa shule ya Roka kuamua kubuni njia mbadala ya kutumia shule yake kujipatia pato la kila siku.

Kulingana na ripoti iliyopeperushwa na runinga ya NTV, Kung’a alieleza kuwa fedha alizokuwa nazo hazingeweza kuyakidhi mahitaji yake kwa zaidi ya mwezi moja, hivyo alifikiri kuhusu njia mbadala.

‘’ Nilianza kuwaza kuhusu la kufanya ili kuwasaidia walimu maana singeweza kuwalipa tena, visa vya corona vikizidi pia kupanda,’’ Kung’u alisema.

Kirinyaga: School owner transforms playground into vegetable farm as COVID-19 effects persist

Baada ya kugundua kuwa hali ya corona haiishi, aliamua kuugeuza uwanja wa shule hiyo kuwa shamba la mboga.

Aliwaambia walimu waliokuwa shuleni humo kuhusu wazo lake na moja kwa moja wakakumbatia.

‘’ Tumekuwa tukifanya ukulima hapa na mwalimu mkuu Moses Wandera ambaye anatoka maeneo ya Magharibi na hakuenda nyumbani maana tulitaka aendeleza masomo ya mtandaoni. Wakati wowote hayuko darasani, anaungana nasi shambani,’’

Kirinyaga: School owner transforms playground into vegetable farm as COVID-19 effects persist

Kando na mboga, Kungu ameitumia uwanja huo kufuga kuku wa kutaga mayai.

Anaeleza kuwa kupitia kwa shamba hilo, walimu wake sasa wanawea kujikimu kimaisha.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/jamaa-ageuza-uwanja-wa-shule-kuwa-shamba-la-mboga-kufuatia-mlipuko-wa-covid19/

No comments:

Post a Comment