Tuesday, July 14, 2020

DPP Mganga amewasimamisha kazi mawakili wawili wa serikali kisa mauaji ya kikongwe

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amewasimamisha kazi mawakili wawili wa serikali mkoani Simiyu baada ya kuwaachia watuhumiwa saba katika kesi ya mauaji ya kikongwe.

DPP Mganga ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari alisema mawakili hao wamewafutia kesi watuhumiwa hao bila kuwepo kwa taarifa ya sababu ya kuifuta kesi hiyo.

Amesema alipatiwa taarifa kuwa washtakiwa wamefutiwa kesi hiyo ambapo awali walitolewa wawili na awamu ya pili wakatolewa watano.

Mganga amesema katika kesi hiyo kuna viashiria vyake rushwa hali ambayo ilimlazimu kufuatilia.

“Kuna ukiukwaji ambao siwezi kunyamaza kuna maelekezo ambayo wakili wa serikali anatakiwa kuyafuata kabla ya kufuta kesi hakuna aliyeandika kesi imefutwa kwa sababu gani,” amesema DPP Mganga

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/dpp-mganga-amewasimamisha-kazi-mawakili-wawili-wa-serikali-kisa-mauaji-ya-kikongwe/

No comments:

Post a Comment