Tuesday, July 14, 2020

Dkt Mwinyi “Sina Wasiwasi na Maalim Seif”

Mchagueni Hussein Mwinyi, Magufuli awaasa WazanzibariMgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Hussein Mwinyi amesema hana wasiwasi juu ushindani atakaoupata toka kwa mgombea urais kwa tiketi ya chama ACT Maalim Seif Hamadi.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha Utv Dkt. Mwinyi amesema ana mheshimu Maalim Seif kutokana na uzoefu wake kwenye siasa za Zanzibar lakini sera za chama chake ni bora zaidi.

“Wanachama ni wale wale na vingozi ni wake wale sidhani kama wanabadilisha chochote bado naamini kuwa sisi tuna sera nzuri kuliko wao na naamini tutashinda” amesema.

Ikumbukwe kuwa Dkt. Mwinyi amechaguliwa na chama chake cha CCM kuwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi ujao utaotarajiwa kufanyika mnamo mwezi Oktoba.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/dkt-mwinyi-sina-wasiwasi-na-maalim-seif/

No comments:

Post a Comment