Tuesday, July 14, 2020

Diamond “Nilijua Vanessa Mdee Anaenda Kuumia”

Diamond Amwagia Sifa Kibao Vanessa Mdee - Ghafla! TanzaniaMwanamzuiki Naseeb Adbul (Diamond) amesema alikuwa akimsikitia msanii mwenzie Vanessa Mdee pindi aliposaini mkataba wa kujiunga na kampuni ya Universal Music kwa ajili ya kusimamia kazi zake za muziki.

Diamond amesema yeye ana uzoefu juu ya mikataba ya makampuni ya kimataifa ya lakini alikaa kimya kwakaua alijua kama angeongea kuhusu ugumu wa kufanya kazi na makampuni hayo angeonekana mbaya mbele za watu.

“Nisiwe mnafiki, Nimefanya kazi na Universal takribani miaka miwili na nusu nimemalizana nao mwaka huu. Nisiwe mnafiki ninapoona msanii yeyote akisaini mara ya kwanza namsikitikia. Dada yangu vanessa mdee alivyosigniwa niliwaambia uongozi kwamba duuh natamani ajue anachoenda kukutana nacho. Lakini mimi sio mtu wa kuongea mitandaoni nakaaga tu kimya” amesema Diamond.

Ikumbukwe mapema mwezi Juni Vanessa Mdee alitangaza kuacha muziki kutokana na tasnia hiyo kujaa na mambo ambayo hayapo hayafurahishi na kutishia uhai wake.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/diamond-nilijua-vanessa-mdee-anaenda-kuumia/

No comments:

Post a Comment