Monday, July 20, 2020

Dondoo za leo; Vigogo wapeta kura za maoni CCM, Mwakyembe apigwa chini, Steve Nyerere afunguka kupata kura 6

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja vigogo wapeta kura ya maoni CCM, Mwakyembe chali na mwisho ni juu ya Steve Nyerere kufunguka baada ya kupata kura 6. Karibu;

VIGOGO WAPETA KURA ZA MAONI CCM

MCHAKATO wa kura za maoni kuwasaka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakaopeperusha bendera ya chama hicho kusaka ubunge na uwakilishi ulianza jana, baadhi ya vigogo wakiendelea kung’ara

Miongoni mwa vigogo waliong’ara ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na Naibu wake, Dk. Tulia Ackson.

Kenye Jimbo la Kongwa, Spika Ndugai ameongoza akipata kura 850 akifuatwa na Dk. Samora Mshanga aliyepata kura 20, Isaya Mngulumi (19), Dk. Philimon Saigod (6), Neemia Chibelenje (2), Apiov Iwiwa (1) na Morice Zaid (0).

Soma zaidi>>>

MWAKYEMBE AANGUKIA PUA

Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, amekuwa mshindi watatu katika uchaguzi wa kura za maoni katika jimbo la Kyela lililopo mkoani Mbeya.

Mwakyembe ambaye alitia nia ya kutetea jimbo la Kyela ambalo amekuwa akiliongoza alipata kura 252 katika matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana.

Soma zaidi>>>

MANENO YA STEVE NYERERE BAADA YA KUPATA KURA 6

“Kwanza nichukue nafasi hii kusema asante Mungu kwa kila jambo, hakika nimeona uwezo wako nimeona nguvu yangu nimeona kipaji changu nimeona jinsi gani Baba anavyonipigania kwenye kila jambo, niseme Asanteni sana Wasanii wenzangu mlionikimbilia kwenye hili”

“Asante marafiki zangu Ndugu zangu pamoja na Waandishi wa habari wote nasema bila nyie mimi siwezi, niseme asante kwa Chama changu Viongozi wote wa Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Ally Hapi, Salim Asas, DC Richard Kasesela na Viongozi na Wanachama wote wa CCM”

Soma zaidi>>>

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/dondoo-za-leo-vigogo-wapeta-kura-za-maoni-ccm-mwakyembe-apingwa-chini-steve-nyerere-afunguka-kupata-kura-6/

No comments:

Post a Comment