Tuesday, July 14, 2020

Dondoo za leo: Ni mafuriko ubunge CCM, Wadhamini wa Lissu wawekewa pingamizi na Sugu aibuka kidedea kura za maoni

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Jumatano Julai 15, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni watu wafurika kugombea ubunge CCM kulikoni? Wadhamini wa Lissu wawekewa pingamizi je unajua ni kwa nini soma habari hizi kwa kina na Sugu aibuka kidedea kura za maoni.

Karibu msomaji wetu;

NI MAFURIKO UBUNGE CCM

Ni mafuriko. Ndicho kinachoonekana katika uchukuaji na urejeshaji fomu za kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge katika majimbo mbalimbali nchini.

Waliojitokeza wengi ni waliowahi kuwa wabunge kwenye majimbo hayo kipindi kilichopita, waliokuwa wabunge hadi Julai, mwaka huu, mawaziri, naibu mawaziri, wanasheria, wasomi na wanataaluma mbalimbali.

Pia katika mchakato huo, wamo waandishi wa habari, wafanyabiashara, wakuu wa zamani wa taasisi nyeti, vijana na viongozi wa ngazi mbalimbali za serikali wakiwamo waliokuwa wakuu wa mikoa.

Soma zaidi

WADHAMINI WA LISSU WAWEKEWA PINGAMIZI

Upande wa Jamhuri umewasilisha pingamizi la awali mahakamani kupinga maombi yaliyowasilishwa na wadhamini Ibrahim Ahmed na Robart Katula wa mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ukidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza na kutaka maombi hayo yatupwe.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wadhamini hao wamefungua maombi wakiitaka itoe hati ya kumkamata Lissu kwa kuwa wao wameshindwa kumpata.

Kesi hiyo imetajwa jana katika mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Soma zaidi

SUGU AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI

Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu amepitishwa kugombea jimbo hilo.

Sugu ameibuka mshindi wa uchaguzi kwenye kura za maoni za ubunge Chadema katika jimbo la Mbeya Mjini kwa kupata kura 294.

Sugu alikuwa ni mgombea pekee na alihitaji kura za ndio au hapana ambapo alipata kura za ndio 294 na hapana 5.

Soma zaidi



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/dondoo-za-leo-ni-mafuriko-ubunge-ccm-wadhamini-wa-lissu-wawekewa-pingamizi-na-sugu-aibuka-kidedea-kura-za-maoni/

No comments:

Post a Comment