Tuesday, July 14, 2020

Sugu aibuka kidedea kura za maoni kugombea Mbeya Mjini

Aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu amepitishwa kugombea jimbo hilo.

Sugu ameibuka mshindi wa uchaguzi kwenye kura za maoni za ubunge Chadema katika jimbo la Mbeya Mjini kwa kupata kura 294.

Sugu alikuwa ni mgombea pekee na alihitaji kura za ndio au hapana ambapo alipata kura za ndio 294 na hapana 5.

Kiongozi huyo aliwashukuru kwa kura alizopigiwa na kusema wameonyesha heshima kubwa kwake.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/sugu-aibuka-kidedea-kura-za-maoni-kugombea-mbeya-mjini/

No comments:

Post a Comment