Tuesday, July 14, 2020

Lema: Kugombea kupitia upinzani ujiandae kufutiwa uraia, kutekwa ama kubambikiwa kesi

Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema kugombea kupitia upinzani ni maisha ya roho mkononi kila wakati.

Amesema unaweza kufutiwa uraia, kubambikiwa kesi, kufilisiwa, kutekwa, kujeruhiliwa, kuuawa na kuteswa kisaikolojia.

Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa ” Ni utitiri wa visa na hofu,”.

“Unashika fomu ya kugombea mkono mmoja na mkono wa pili unaandika wosia,” aliandika Lema.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/lema-kugombea-kupitia-upinzani-ujiandae-kufutiwa-uraia-kutekwa-ama-kubambikiwa-kesi/

No comments:

Post a Comment