Monday, July 13, 2020

Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kuua mkewe na watoto

Mkazi wa Katavi, Yustine Robert (35) amehukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga  baada ya kupatikana na hatia ya kumuuwa mke na watoto wawili.

Akisoma hukumu hiyo jana  Jaji Mfawidhi Wa Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga David Mrango, alisema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo katika eneo la majiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Aprili 5, 2013 kwa kuwatupa kwenye kisima cha maji mke wake na watoto wake wawili.

Ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa mashitaka ulionesha kuwa mtuhumiwa alikuwa na ugomvi wa kifamilia siku moja kabla ya vifo vya wanafamilia wake.

Mrango alieleza kuwa mashahidi hao walisema kuwa mtuhumiwa alisikika akisema atafanya tendo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika eneo hilo.

Jaji  alisema ushahidi ambao umemtia hatiani Yustine Robert ni ushahidi wa kimazingira ambao umetosha kuthibitisha shitaka aliloshitakiwa nalo mtuhumiwa.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Jaji Mrango alimhukuku mtuhumiwa huyo kunyongwa hadi kufa kutokana na mauaji hayo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/ahukumiwa-kunyongwa-hadi-kufa-baada-ya-kuua-mkewe-na-watoto/

No comments:

Post a Comment