Wengi tunakula mapera kama tunda pasi kujua kuwa tunda hilo lina manufaa ya ajabu kiafya. Jarida la Bongo Leo limefanya utafiti zaidi na kubaini kuwa tunda la mpera lina manufaa si haba kiafya
Haya ndiyo baadhi ya manufaa ya kiafya ya ulaji wa mapera na majani yake:
-Huimarisha afya ya moyo. Moyo ni kiungo muhimu zaidi mwilini na kila unapopata madhara, mwili mzima huwa na tatizo ama hata kusababisha kifo, maana ndiyo husaidia katika kupiga damu.
Ulaji wa mapera husaidia katika kuimarisha afya ya moyo na kuifanya kupiga damu ipasavyo.
– Hupunguza uchungu wa hedhi- Asilimia kubwa wanawake huwa na wakati mgumu wakati wa hedhi, utafiti umebaini kuwa ulaji wa mapera hupunguza uchungu huo kwa kiwango kikubwa. Mtu huweza kuyafuna majani yake ama kuchemsha kasha kuyanywa maji hayo.
– kusaidia katika usagaji wa chakula – Mapera yana umuhimu mkubwa katika kusaidia kusaga chakula tumboni. Kando na hivyo, matumizi ya majani yake hutibu ugonjwa wa kuendesha.
– Kupunguza uzani. Ulaji wa mapera ni suluhu kamili kwa yeyote anayetaka kupunguza uzani wa mwili. Unapokula mapera, unajihisi kuwa tumbo limejaa , hii ni kutokana na calories zake na hivyo kupunguza uzani pakubwa.
– Kuzuia saratani. Utafiti umebaini kuwa ulaji wa mapera hupunguza kwa kiwango kikubwa nafasi ya kupata maradhi ya saratani. Hii ni kwa sababu ina uwezo wa kuivinja seli zake.
-Kuimarisha kinga ya mwili. Mapera yana vitamin C ambayo ndiyo huukinga mwili dhidi ya maradhi.
Kulainisha ngozi- ulaji wa mapera hunyoosha na kulainisha ngozi ya mwili na kukuacha kwa ngozi yenye afya.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/faida-7-za-kiafya-za-mapera-majani-yake-ni-dawa/
No comments:
Post a Comment