Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, wametangaza kuchukua fomu leo ya kugombea katika majimbo yao waliyokuwa wanayaongoza.
Lema amesema leo majina ya saa tano atakwenda kuchukua fomu ya kuendelea kuwa mbunge wa Arusha Mjini 2020 hadi 2025.
Kesho tarehe 9/7/2020 nitachukua fomu ya kuendelea kuwa Mbunge wa Arusha Mjini 2020 – 2025 tena. Ni katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Kaskazini,saa tano asubuhi.
— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) July 8, 2020
Heche amesema atachukua fomu kwa ajili ya kuongoza jimbo lake la Tarime vijijini.
“Tuko tayari kuendelea kuifanya kazi ya kujenga taifa la demokrasia linaloheshimu utu, haki, usawa na ustawi wa watu,” aliandika Heche.
Kesho nitachukua fomu ndani ya chama changu kuanza mchakato wa kutetea nafasi yangu ya kuendelea kuongoza jimbo la Tarime Vijijini.
Tuko tayari kuendelea kuifanya kazi ya kujenga Taifa la kidemokrasia linaloheshimu utu,haki, usawa na ustawi wa watu.— John Heche (@HecheJohn) July 8, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/lema-na-heche-leo-kuchukua-fomu-za-kugombea-ubunge-wasema-wanarudi-walipokuwa/
No comments:
Post a Comment