Tuesday, July 14, 2020

Dkt Mwinyi Amkana Baba Yake Kumsaidia kushinda Kugombea Urais

Ali Hassan Mwinyi: Tanzania sio kichwa cha mwenda wazimu - YouTubeMgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Hussein Mwinyi amesema baba yake mzazi aliyekuwa rais wa awamu ya Tatu Ali Hassan Mwinyi hakutimika kumpigia kampeni  ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) wakati akitia nia ya kugombea urais ndani ya chama.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum na mtangazaji wa kituo cha Televisheni  cha UTV Tido Mhando amesema baba yake ajilitenga mbali na swala hilo ili kuleta demokrasia ndani ya chama

“Naweza kusema baba yangu alikaa mbali kabisa na hata kufanya mahojiano na watu nilipomueleza tu nia yangu tuliongea tu nyumbani na baada ya hapo akaa kimya alijizuia asiongee na mtu ili asije akasema kitu cha tofauti” amesema.

Ikumbukwe kuwa Dkt. Mwinyi amechaguliwa na chama chake cha CCM kuwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi ujao utaotarajiwa kufanyika mnamo mwezi Oktoba.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/dkt-mwinyi-amkana-baba-yake-kumsaidia-kushinda-kugombea-urais/

No comments:

Post a Comment