Tuesday, July 14, 2020

Mapenzi:  Mwanamke Afunga Harusi na Mume Hospitalini Baada ya Kuhusika Kwenye Ajali Mbaya

BBC News.

Gabin Ndayiziye alihusika katika ajali ya barabara ambayo iliacha mwili wake umeponza tangu Juni 30

Wawili hao walikuwa wamepanga kufunga harusi Julai 4 lakini ajali hiyo ikavuruga mipango

Bibi harusi alizungumza na mchungji kuhusu uwezekano wa kuendelea na harusi, alikubali

Mwanadada mmoja raia wa Burundi amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kuchukua hatua ya kufunga pingu za maisha na mumewe hospitalini baada ya kuhusika katika ajali mbaya.

Charlotte Mukantwari aliamua kuendelea na shughuli ya mipango ya harusi licha ya mumewe kuvunja katika ajali na mwili wake kuponza.

Harusi hiyo ilipangwa kufanyika Julai 4. Bwana harusi alihusika katika ajali hiyo mbaya Juni 30.

‘’ Nimekuwa nikiisubiri siku hiyo, kupatana na changamoto ilikuwa kama majaribu, singeweza kufikiri kuhusu jinsi maisha yangu yangekuwa baada ya kukosa kufanyika hafla hiyo,’’ alisema.

BBC News.

Baada ya kuzungumza na mchungaji kuhusu kundelea na harusi hiyo hospitalini, Charlotte alimthibitishia mpenziwe mapenzi kamili kwa kumfungisha pingu za maisha, harusi hiyo ikifanyika katika hospitali ya Kirundoa alikolazwa.

Siku ilifika, jamaa na marafiki walifika hospitalani humo wakiwa na zawadi kadhaa kushuhudia wawili hao wakifunga pingu za maisha.

Sherehe ikawa fupi na ya kupendeza, mapenzi ya kweli yakadhihirika wazi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/mapenzi-mwanamke-afunga-harusi-na-mume-hospitalini-baada-ya-kuhusika-kwenye-ajali-mbaya/

No comments:

Post a Comment