Wednesday, July 15, 2020

ACT Kumtambulisha Membe Kesho

ImageKiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameweka wazi kuwa kesho Julai 16, 2020 watambambulisha rasmi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho baada ya kufukuzwa na chama cjhake cha zamani (CCM).

Zitto ameweka wazi hayo kwenye ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa ameweka picha ya Membe hukua akiwa ameshikiria kitabu cha ACT-Wazalendo.

Kwa muda mrefu sasa Bernard Mmebe amekuwa kihusishwa na kuhamiakwenye chama cha ACT wazalendo baada ya kufukuzwa CCM baada ya kukiuka baadhi ya taratibu za chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mwanahalisi mmebe atatambulishwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa mlimani City Julai 15, mbele ya wanchama wa chama hicho.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/act-kumtambulisha-membe-kesho/

No comments:

Post a Comment