Tuesday, July 14, 2020

Aggrey Mwanri Ajitosa Ubunge Siha

ImageAliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais maoema mwezi Oktoba.

Mwanri ambaye alitangaza kustaafu ukuu wa mkoa amechukia dili hiyo leo Julai 14,2020 kwenye ofisi za chama hicho mkoani Kilimanjaro.

Mwanri kabla ya kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora alikuwa mbunge wa jimbo ka Siha kwanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015 kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) na kushijka nyadhifa mbalimbali akiwemo ya kuwa naibu waziri wa TAMISEMI.

Ikumbukwe mapema Julai3, 2020 Rais John Magufuli alitangaza kuteua mkuu wa mkoa mpya wa tabora baada ya Aggrey Mwanri kutangaza kustaafu nafasi hiyo aliyohudumu kwa miaka mitano.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/aggrey-mwanri-ajitosa-kuchukua-fomu-ubunge-siha/

No comments:

Post a Comment