Kwa zaidi ya miezi sita, WHO limesisitiza kuwa virusi vya corona husambazwa tu kutokana na matone ya aliyeambukizwa na wala si kupitia kwa hewa
Kundi la watafiti sasa wamebaini kuwa matone hayo huweza kusalia hewani na mtu yeyote huweza kuzipata kwa njia hiyo
Wamelitaka WHO kujumuisha hewa kama njia mojawapo ambayo kwayo virusi hivyo husambaa.
Shirika la afya ulimwenguni WHO sasa limebaini kuwa hewa huenda ikawa njia mojawapo ambako virusi vya corona huweza kusambaa kwazo.
Maria Van Kerkhove, ambaye ni moja wa watafiti na viongozi wa shirika la WHO alieleza kuwa kundi la wanasayansi walioufanya utafiti huo liliwabainishia hilo na kuwa WHO hivi karibuni itatoa habari zaidi kuhusu jinsi virusi hivyo vya corona huweza kusambaa kupitia kwa hewa.
‘’ Tumekuwa tukizungumza kuhusu uwezekano wa virusi vya corona kusambaa kupitia kwa hewa,’’ Kerkhove alisema.
Tangu virusi vya corona vilipolipuka kwa mara ya kwanza Wuhan na baadaye kutangazwa kama janga la ulimwengu, shirika hilo limeshikilia kuwa virusi hivyo huweza kusambaa tu kupitia kwa matone ya mdomo na pua ya aliyeambukizwa.
Wanasayansi hao sasa wamebaini kuwa kuna uwezekano wa matone hayo kusalia hewani kwa muda na hivyo kumuambikiza yeyote anayetangamana nayo badaye. Hii ni kupitia kwa mdomo na pua wa mtu anapojishika sehemu hizo.
Wanasayansi wengine nao wameshikilia kuwa virusi hivyo huweza kusambaa zaidi ya mita 1.5 na kusababisa maambukizi haswa kukiwa na hewa.
Aidha, kiongozi huyo wa WHO ameeleza kuwa virusi vya corona huweza kusambaa kwa njia ya hewa haswa katika maeneo ambayo watu wamebanana. Amesisitiza kuwa uvaaji wa barako ni njia kamili ya kujikinga na usambazaji wa virusi hivyo.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/who-yafichua-hatari-mpya-kuhusiana-na-covid19-wananchi-wajihadhari/
No comments:
Post a Comment