Monday, July 13, 2020

Ndege ya Jeshi Yaanguka,  2 Wafariki Papo Hapo

Kenya to receive 6 military choppers from US

Ndege ya Jeshi laanguka Masinga,  2 wafariki

Ngee hiyo ya jeshi ilianguka katika eneo la Masinga na kuwaua wanajeshi wawili papo hapo

Haijabainika kiini cha ajali hiyo

Ndege hiyo ni kati ya ndege saba zilizonunuliwa kutoka Marekani kutumika na  jeshi la Kenya

Wanajeshi wawili wameripotiwa kufariki baada ya ndege walimokuwa wakisafiria kuanguka ghafla katika eneo la Masinga kaunti ya Machakos.

Ndege hiyo aina ya elikopta iliyonunuliwa kutoka Marekani ilianguka mwendo wa 10am Jumatatu, Julai 13, chanzo cha ajali hiyo ikikosa kubainika hadi sasa.

Elikopta  hiyo ya kivita aina MD 530F ni kati ya ndege saba zilizonunuliwa kutoka Marekani kutumika na  jeshi la Kenya.

#MDHelicopters is honored to have been awarded a CLS and Training Contract to support Kenya Defense Forces recent order…

Posted by MD Helicopters, Inc. on Monday, 16 September 2019

Ndege hiyo iliyohusika katika ajali mbaya ni kati ya ndege zingine 12 zilizoagizwa kutoka Marekani kutumika dhidi ya wanamgambo wa Alshaabab.

Ndege hizo ziliwasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa jeshi Jenerali Samson Mwathethe katika hafla iliyohudhuriwa na balozi wa Amerika nchini Kenya Kyle McCarter.

Ajali hii inajiri mwezi mmoja tu baada ya ndege nyingine ya elikopta ya polisi kulazimika kutua ghafla katika shamba la ndizi katika kaunti ya Meru.

Mamlaka ya kusimamia usafiri wa ndege nchini KCAA pamoja na kitengo cha polisi zimeanza uchungzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/ndege-ya-jeshi-yaanguka-2-wafariki-papo-hapo/

No comments:

Post a Comment