Monday, July 20, 2020

Mtangazaji Zamaradi Mketema aambulia kura mbili jimbo la Kinondoni

Mtangazaji na mwanaharakati, Zamaradi Mketema amepata kura mbili katika uchaguzi wa kura za maoni kwa wagombea wa jimbo la Kinondoni.

Akijinadi leo wakati akiomba kura Zamaradi alisema kuwa sifa ambazo zimetajwa na katibu dhidi ya anayegombea ni kwamba anazo.

“Sifa zote ninazo mbali na hivyo nashaurika, nafikika, naingilika naomba mnipe kura niweze kulisongesha gurudumu la maendeleo Kinondoni,” amesema Zamaradi

Mbunge anayemaliza muda wake jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, Maulid Mtulia ameshindwa kutetea nafasi yake katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujikuta akiambulia kura 11.

Mtulia ameangushwa na Abbas Tarimba katika kura hizo za maoni zilizofanyika leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 katika Ukumbi wa King Solomon.

Wagombea walikuwa 79 ambapo Tarimba amepata kura 171, mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Iddi Azzan kura 77 na Mtulia kura 11 kati ya kura zote 404 zilizopigwa na wajumbe wote huku wengine wakiambulia kura moja na mbili.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/mtangazaji-zamaradi-mketema-aambulia-kura-mbili-jimbo-la-kinondoni/

No comments:

Post a Comment